Orodha ya Kampuni za Kubeti zenye Leseni Tanzania

Orodha kamili ya kampuni 38 za kubeti mtandaoni zenye leseni ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, kama ilivyokaguliwa tarehe 5 Novemba 2026.

Imekaguliwa mara ya mwisho: 5 Novemba 2026. Chanzo: rejista ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

Kabla ya kufungua akaunti kwenye tovuti yoyote ya kubeti, hakikisha kampuni hiyo ina leseni ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Kampuni yenye leseni inasimamiwa na sheria za Tanzania: inapaswa kulinda pesa zako, kuthibitisha umri wa wateja na kukupa njia ya kulalamika ikiwa kuna tatizo.

Hapa chini kuna orodha ya kampuni zote zilizo kwenye rejista ya GBT ya kubeti mtandaoni (online sports betting). Tumeinakili moja kwa moja kutoka kwenye tovuti rasmi ya Bodi. Tunaikagua tena mwanzoni mwa kila mwezi.

Kampuni 38 zenye leseni ya kubeti mtandaoni

Na.Jina la biasharaKampuni iliyosajiliwa
11WinInteractive Sports Entertainment Company Limited
21XBetKatavi Gaming Limited
3888 BetPort Achia Tanzania Limited
4BangbetBahatisha Basi Tanzania Ltd
5BetikaPaladin & Associates Company Ltd
6Betkumi LimitedBetkumi Limited
7BetPawaChoplife Gaming Limited
8BetsasaALBC Group Limited
9BetwayMedia Bay Limited
10Betwin LimitedBetwin Limited
11BetwinnerBellatrix Media Ltd
12Biko SportMobibet Company Limited
13Blockdance Africa LimitedBlockdance Africa Limited
14Bonanza GamingBonanza Gaming Tanzania
15BongoBongo BetSolner Ltd
16Bookee BetThe Gaming Plug Limited
17Chopbet Company LimitedChopbet Company Limited
18Gals Sport BettingFido Technologies Ltd
19Gama Gaming LimitedGama Gaming Limited
20Gwala BetWhiteball Company Limited
21Hela BetCheza IT Solutions Limited
22King BetJx Betting (T) Limited
23Leon BetSandstorm Company Limited
24Meridian BetBit Tech Limited
25Moja Digital Services Tanzania LimitedMoja Digital Services Tanzania Limited
26Msport Tech LimitedMsport Tech Limited
27ParimatchUltimate Gaming System Limited
28Piccadilly Holding Company (T) LtdPiccadilly Holding Company (T) Ltd
29Piga BetDunia Investment Limited
30PM BetPlaymaster Gaming Corporation Limited
31Premier BetEntertainment Africa Limited
32Soka BetDigital Gaming Solutions Limited
33Sport PesaNexis Global Limited
34Sporty BetMarawin Limited
35Tembo BetBetX Limited
36Throne BetThrone Bet Ltd
37Wasafi BetWasafi Bet Company Limited
38WiBetCleopatra Gaming (T) Ltd

Kumbuka: kwenye rejista ya Bodi, jina la Parimatch limeandikwa “Parimacth”. Hapa tumeandika jina la biashara kama linavyojulikana.

Jinsi ya kusoma orodha hii

  • Jina la biashara ni jina unaloliona kwenye tovuti au app, kwa mfano SportPesa au Betway.
  • Kampuni iliyosajiliwa ni jina rasmi la kampuni yenye leseni. Mara nyingi utaliona chini kabisa ya tovuti ya kampuni ya kubeti (footer) au kwenye vigezo na masharti.
  • Baadhi ya kampuni zinaonekana kwa jina la kampuni tu, bila jina tofauti la biashara. Hivyo ndivyo zilivyoandikwa kwenye rejista.

Leseni ya kubeti si sawa na leseni ya kasino

Bodi ina rejista mbili tofauti: moja ya kubeti michezo na nyingine ya kasino. Kampuni kadhaa zina leseni zote mbili, lakini si kila kampuni. Kwa mfano, kwa mujibu wa rejista ya tarehe 5 Novemba 2026, 1XBet na 1Win zimeorodheshwa kwenye orodha ya kubeti mtandaoni tu, si ya kasino mtandaoni. Ukitaka kucheza michezo ya kasino, angalia rejista ya kasino ya Bodi pia.

Leseni ya maduka ya kubetia (land-based) haitoshi kwa kubeti mtandaoni

Rejista ya Bodi pia ina kampuni nane zenye leseni ya kubeti kwenye maduka (land-based). Leseni hiyo inahusu vituo vya kubetia, si tovuti. Ili kuendesha biashara ya kubeti mtandaoni, kampuni inapaswa kuwa kwenye orodha ya kubeti mtandaoni iliyo hapo juu.

Jinsi ya kuhakiki leseni wewe mwenyewe

  1. Fungua tovuti rasmi ya Bodi: gamingboard.go.tz, sehemu ya leseni (License Operators), kisha chagua “Sports Betting”.
  2. Tafuta jina la kampuni au jina la biashara.
  3. Linganisha jina la kampuni lililo chini ya tovuti ya kubeti na jina lililo kwenye rejista.
  4. Ikiwa jina halipo, usiweke pesa. Ukitumia tovuti isiyo na leseni ya Tanzania, huenda usipate ulinzi wa sheria za Tanzania.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Kuna kampuni ngapi za kubeti zenye leseni Tanzania? Kwa mujibu wa rejista ya Bodi ya tarehe 5 Novemba 2026, kuna kampuni 38 zenye leseni ya kubeti mtandaoni na kampuni 8 zenye leseni ya maduka ya kubetia.

Je, kubeti kwenye kampuni yenye leseni kunamaanisha nitashinda? Hapana. Leseni inahusu usalama na usimamizi wa kampuni, si nafasi yako ya kushinda. Kila dau lina hatari ya kupoteza pesa.

Je, orodha hii hubadilika? Ndiyo. Kampuni mpya zinaweza kupewa leseni, na nyingine zinaweza kuondolewa kwenye rejista. Ndiyo sababu tunaandika tarehe ya ukaguzi mwanzoni mwa ukurasa huu.

Kubeti ni kwa watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi. Weka dau la kiasi tu ambacho unaweza kumudu kukipoteza.