Imekaguliwa mara ya mwisho: 5 Novemba 2026. Chanzo: rejista ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).
Kabla ya kufungua akaunti kwenye tovuti yoyote ya kubeti, hakikisha kampuni hiyo ina leseni ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Kampuni yenye leseni inasimamiwa na sheria za Tanzania: inapaswa kulinda pesa zako, kuthibitisha umri wa wateja na kukupa njia ya kulalamika ikiwa kuna tatizo.
Hapa chini kuna orodha ya kampuni zote zilizo kwenye rejista ya GBT ya kubeti mtandaoni (online sports betting). Tumeinakili moja kwa moja kutoka kwenye tovuti rasmi ya Bodi. Tunaikagua tena mwanzoni mwa kila mwezi.
Kampuni 38 zenye leseni ya kubeti mtandaoni
| Na. | Jina la biashara | Kampuni iliyosajiliwa |
|---|---|---|
| 1 | 1Win | Interactive Sports Entertainment Company Limited |
| 2 | 1XBet | Katavi Gaming Limited |
| 3 | 888 Bet | Port Achia Tanzania Limited |
| 4 | Bangbet | Bahatisha Basi Tanzania Ltd |
| 5 | Betika | Paladin & Associates Company Ltd |
| 6 | Betkumi Limited | Betkumi Limited |
| 7 | BetPawa | Choplife Gaming Limited |
| 8 | Betsasa | ALBC Group Limited |
| 9 | Betway | Media Bay Limited |
| 10 | Betwin Limited | Betwin Limited |
| 11 | Betwinner | Bellatrix Media Ltd |
| 12 | Biko Sport | Mobibet Company Limited |
| 13 | Blockdance Africa Limited | Blockdance Africa Limited |
| 14 | Bonanza Gaming | Bonanza Gaming Tanzania |
| 15 | BongoBongo Bet | Solner Ltd |
| 16 | Bookee Bet | The Gaming Plug Limited |
| 17 | Chopbet Company Limited | Chopbet Company Limited |
| 18 | Gals Sport Betting | Fido Technologies Ltd |
| 19 | Gama Gaming Limited | Gama Gaming Limited |
| 20 | Gwala Bet | Whiteball Company Limited |
| 21 | Hela Bet | Cheza IT Solutions Limited |
| 22 | King Bet | Jx Betting (T) Limited |
| 23 | Leon Bet | Sandstorm Company Limited |
| 24 | Meridian Bet | Bit Tech Limited |
| 25 | Moja Digital Services Tanzania Limited | Moja Digital Services Tanzania Limited |
| 26 | Msport Tech Limited | Msport Tech Limited |
| 27 | Parimatch | Ultimate Gaming System Limited |
| 28 | Piccadilly Holding Company (T) Ltd | Piccadilly Holding Company (T) Ltd |
| 29 | Piga Bet | Dunia Investment Limited |
| 30 | PM Bet | Playmaster Gaming Corporation Limited |
| 31 | Premier Bet | Entertainment Africa Limited |
| 32 | Soka Bet | Digital Gaming Solutions Limited |
| 33 | Sport Pesa | Nexis Global Limited |
| 34 | Sporty Bet | Marawin Limited |
| 35 | Tembo Bet | BetX Limited |
| 36 | Throne Bet | Throne Bet Ltd |
| 37 | Wasafi Bet | Wasafi Bet Company Limited |
| 38 | WiBet | Cleopatra Gaming (T) Ltd |
Kumbuka: kwenye rejista ya Bodi, jina la Parimatch limeandikwa “Parimacth”. Hapa tumeandika jina la biashara kama linavyojulikana.
Jinsi ya kusoma orodha hii
- Jina la biashara ni jina unaloliona kwenye tovuti au app, kwa mfano SportPesa au Betway.
- Kampuni iliyosajiliwa ni jina rasmi la kampuni yenye leseni. Mara nyingi utaliona chini kabisa ya tovuti ya kampuni ya kubeti (footer) au kwenye vigezo na masharti.
- Baadhi ya kampuni zinaonekana kwa jina la kampuni tu, bila jina tofauti la biashara. Hivyo ndivyo zilivyoandikwa kwenye rejista.
Leseni ya kubeti si sawa na leseni ya kasino
Bodi ina rejista mbili tofauti: moja ya kubeti michezo na nyingine ya kasino. Kampuni kadhaa zina leseni zote mbili, lakini si kila kampuni. Kwa mfano, kwa mujibu wa rejista ya tarehe 5 Novemba 2026, 1XBet na 1Win zimeorodheshwa kwenye orodha ya kubeti mtandaoni tu, si ya kasino mtandaoni. Ukitaka kucheza michezo ya kasino, angalia rejista ya kasino ya Bodi pia.
Leseni ya maduka ya kubetia (land-based) haitoshi kwa kubeti mtandaoni
Rejista ya Bodi pia ina kampuni nane zenye leseni ya kubeti kwenye maduka (land-based). Leseni hiyo inahusu vituo vya kubetia, si tovuti. Ili kuendesha biashara ya kubeti mtandaoni, kampuni inapaswa kuwa kwenye orodha ya kubeti mtandaoni iliyo hapo juu.
Jinsi ya kuhakiki leseni wewe mwenyewe
- Fungua tovuti rasmi ya Bodi: gamingboard.go.tz, sehemu ya leseni (License Operators), kisha chagua “Sports Betting”.
- Tafuta jina la kampuni au jina la biashara.
- Linganisha jina la kampuni lililo chini ya tovuti ya kubeti na jina lililo kwenye rejista.
- Ikiwa jina halipo, usiweke pesa. Ukitumia tovuti isiyo na leseni ya Tanzania, huenda usipate ulinzi wa sheria za Tanzania.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Kuna kampuni ngapi za kubeti zenye leseni Tanzania? Kwa mujibu wa rejista ya Bodi ya tarehe 5 Novemba 2026, kuna kampuni 38 zenye leseni ya kubeti mtandaoni na kampuni 8 zenye leseni ya maduka ya kubetia.
Je, kubeti kwenye kampuni yenye leseni kunamaanisha nitashinda? Hapana. Leseni inahusu usalama na usimamizi wa kampuni, si nafasi yako ya kushinda. Kila dau lina hatari ya kupoteza pesa.
Je, orodha hii hubadilika? Ndiyo. Kampuni mpya zinaweza kupewa leseni, na nyingine zinaweza kuondolewa kwenye rejista. Ndiyo sababu tunaandika tarehe ya ukaguzi mwanzoni mwa ukurasa huu.
Kubeti ni kwa watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi. Weka dau la kiasi tu ambacho unaweza kumudu kukipoteza.